Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, January 28, 2014

UN:Rwanda inawakandamiza wapinzani

Afisaa mmoja mkuu katika Umoja wa mataifa, amekosoa ambavyo serikali ya Rwanda inawatendea wanasiasa wa upinzani.
Mwanasiasa wa upinzani Victoire Ingabire amefungwa jela kwa kupinga serikali ya Kagame
Akiongea na BBC, wiki moja baada ya ziara yake nchini humo, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, Maina Kiai alisema kuwa karibu kila mwanasiasa, anayejitokeza hadharani kupinga serikali, huishia kwenye matatizo ya kisheria.
Baadhi hukamatwa na kufungwa jela kwa kile kinachosemekana kuwa kueneza uvumi.
Bwana Kiai alisema kwamba alizungumza na mwanamume mmoja akiwa gerezani kuhusu siasa.
Kiai amesema kuwa angali anafanya mazungumzo ya kina na serikali ya Rwanda kuhusu hilo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment