Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, January 1, 2014

TAARIFA ZA KIFO CHA WAZIRI WA FEDHA MH:MGIMWA KWA AWALI ZIPO HAPA

 
Aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr.Stephen Mgimwa amefariki dunia asubuhi ya leo, nchini Afrika ya kusini alikokua akipata matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu..!!

Tanzia Waziri wa Fedha William Mgimwa, Mb

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Waziri wetu wa Fedha ndg. William Mgimwa.
Kwa kipindi kifupi nilichofanya naye kazi kwa karibu, kwanza kwenye Kamati ya Fedha (nikiwa mkaribishwa kama Waziri wa Fedha kivuli), kisha kwenye kamati ndogo niliyounda kuhusu miradi ya Umeme ya Mchuchuma na Liganga na Ngaka, na baadaye akiwa Waziri wa Fedha, jambo la msingi nilioona kwake ni unyenyekevu na heshima kubwa aliyonayo kwa watu wengine. Hakusita kuomba ushauri licha ya kuwa na tofauti za kivyama na kwa kweli ni Waziri wa Fedha niliyeelewana naye zaidi kuliko wengine wote waliopita nikiwa ama Waziri Kivuli au Mwenyekiti wa Kamati za Mahesabu. Uzalendo wake hauna mashaka na kujituma kwake katika kazi ni tabia ya kupigiwa mfano.
Mungu ameamua kumchukua mja wake na sisi wanadamu hatuna uwezo wa kupinga. Nawapa pole sana familia yake kwa kumpoteza baba yao mpendwa. Naomba mola awape moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kalenga na Halmashauri ya Wilaya Iringa kwa kupoteza kiongozi wao.
Mola ailaze Roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment