Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, January 26, 2014

Maadhimisho yapita kwa kishindo Misri

Waandamanaji kadha wameuwawa katika mapambano yaliyotokea mjini Cairo na miji mengine ya Misri, wakati maandamano ya pande zinazopingana yamefanywa kuadhimisha mwaka wa tatu wa maandamano yaliyompindua Hosni Mubarak.Wafuasi wa jeshi wakiandamana medani ya Tahrir
Mjini Cairo polisi walitumia moshi wa kutoza machozi na kufyatua risasi hewani kuwatawanya wanaharakati walioandamana na waandamanaji Waislamu wanaomuunga mkono rais wa zamani Mohamed Morsi ambaye alitolewa madarakani na jeshi.
Inaarifiwa kuwa bomu lilotegwa kwenye gari liliripuka karibu na kambi ya polisi katika mji wa Suez.
Wafuasi wa serikali piya walikusanyika katika medani ya Tahrir kuadhimisha siku hiyo, wakipiga kelele huku wamebeba picha za mkuu wa jeshi, Jenerali Abdul Fattah al-Sisi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment