Writen by
sadataley
11:54 AM
-
0
Comments
Na Joseph Zablon, Mwananchi
Dar es Salaam. Moto umezuka kwenye ghala la kuhifadhia dawa za binadamu ambalo pia ni Hifadhi ya Taifa ya Viinilishe ambalo linamilikiwa na Philips Pharmaceuticals, lililopo eneo la Vingunguti na kuteketeza mali zilizokuwemo humo.
Tukio hilo limetokea jana saa 9 alasiri na kuzua hofu kubwa wafanyakazi katika majengo ya jirani na wapita njia.
Hofu kubwa zaidi katika eneo hilo ilitanda hasa kufuatia ghala hilo kuwa karibu na Kituo cha Mafuta cha Victoria.
“Mafundi walikuwa wakifanyakazi juu ya paa mara tukaona moto unazuka,” alisema mmoja wa mashuhuda ambaye alijitambulisha kwa jina la Ramadhani Lugano mfanyakazi wa karakarana mojawapo jirani na ghala hilo.
Aliongeza: “Hatufahamu sababu, lakini juu ya ghala kulikuwa na mafundi wakiendelea na kazi, na ndiko moto ulipoanzia kabla ya kusambaa sehemu zingine za ghala hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi walifika eneo la tukio muda mfupi baadaye.
“Chanzo inawezekana ikawa hitilafu ya umeme, kwani moto ulianza katika paa ambako mafundi walikuwa wakifanya kazi,” alisema
Vikosi vya kupambana na moto vilifika mara moja eneo la tukio na kuanza kazi ya kuuzima moto huo.Alisema kuwa moto ulidhibitiwa kwa kiasi kikubwa na mkazo ulikuwa kuhakikisha haufiki katika kituo cha mafuta cha Victoria kuepusha madhara makubwa.
“Zimatoto wamefanya kazi kubwa kuudhibiti moto kuendelea kuteketeza ghala na mali zilizopo ndani. Hii ni kwa sababu walifika eneo la tukio mapema na kuanza kuudhibiti moto huo,” alisema zaidi.
“Hatujui viinilishe kiasi gani vimeharibiwa na moto na hata hasara ya jumla,” alisema Sadiki na kuongeza:
“Viinilishe ambavyo vimeteketezwa ni vile ambavyo vipo katika mpango uliozinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete.
Alisema Rais Kikwete, hivi karibuni alizindua mpango wa kuwekwa viinilishe katika vyakula, na ghala hilo liliteuliwa kuhifadhi viinilishe hivyo.
No comments
Post a Comment