Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, December 28, 2013

Simba, Yanga zafukuza makocha tisa miaka mitatu

Ernest Brandts.PICHA|MAKTABA 
Na Sosthenes Nyoni, Mwananchi
Dar es Salaam. Wakati Yanga imesitisha mkataba wa kazi wa kocha wake, Ernest Brandts imebainika kuwa Yanga na Simba zimefukuza makocha tisa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Simba ndiyo inayoongoza kwa kuwatimua makocha watano wakati Yanga imefungisha virago makocha wanne kuanzia 2010 hadi 2013.
Makocha waliokumbwa na mkasa wa kutimuliwa kwa upande wa Simba ni Patrick Phiri (Zambia), Milovan Cirkovic (Serbia), Moses Basena (Uganda), Patrick Liewig (Ufaransa) na Mtanzania pekee Abdallah Kibadeni.
Yanga iliwatimua Sam Timbe (Uganda), Kostadin Papic (Serbia), Tom Saint Fiet (Ubelgiji) na Ernest Brandts kutoka Uholanzi.
Kwa kuanzia na Phiri (56) aliteuliwa kuifundisha Simba Septemba 9,2009 na akatimuliwa Aprili 19, 2011 huku akiwa amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili 2004-5 na 2009-10, Kombe la Tusker 2005 na Kombe la Kagame 2006.
Baada ya Phiri kuondolewa, Simba ilimtwaa Basena ambaye alidumu kwa muda wa miezi sita pekee baada ya kusitishiwa mkataba Novemba mwaka huohuo na nafasi yake kuchukuliwa na Milovan aliyeiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kuifikisha timu hiyo katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Licha ya kuifikisha Simba katika hatua ya 16 bora ilipofika Oktoba 2012 Milovan aliondolewa na nafasi yake ilichukuliwa na Liewig ambaye naye alilazimishwa kukusanya kila kilicho chake Juni mwaka huu na kumkabidhi majukumu Kibadeni aliyefurushwa mara tu baada ya mzunguko wa kwanza kukamilika Novemba mwaka huu.
Katika kipindi hicho, Yanga ilikuwa hivi, Timbe aliyeiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa ligi na Kombe la Kagame alitimuliwa Novemba 2012 na nafasi yake ikachukuliwa na Papic ambaye Mei mwaka jana mkataba wake ulisitishwa na nafasi yake ikachukuliwa na Saintfiet ambaye alipigwa chini miezi mitatu baadaye na timu kukabidhiwa kwa Brandts aliyesitishiwa mkataba siku chache zilizopita.
Hivi sasa Simba iko chini ya Kocha mpya, Zdvacko Logarusic kutoka Croatia na Yanga iko katika mchakato wa kutafuta kocha mpya huku ikimwondoa kocha msaidizi, Fred Felix Minziro na nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na Boniface Mkwasa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment