Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, December 28, 2013

Ni vigumu kusitishwa vita Sudan K

Wakati juhudi zikizidi kuendelea za kujaribu kumaliza mapigano Sudan Kusini, Msemaji wa Jeshi la Sudan Kusini amesema kuna matumaini madogo ya kusitishwa kwa mapigano.
Wanajeshi wakiwaondoa raia wa Sudan Kusini kutokana na mapigano yanayoendelea
Kiongozi wa waasi Riek Machar amesema wapiganaji wake bado wanashikilia eneo kubwa la Kaskazini mwa nchi, huku majeshi ya serikali yakisema yameukomboa mji wa Malakal na wamezingira eneo la Bentiu , mji mkuu wa jimbo la Unity.
Rais Salva Kiir amesema yupo tayari kusitisha mapigano mara moja, lakini hasimu wake Bwana Machar amesema mazungumzo zaidi yanahitajika kukubaliana kusitisha mapigano na kwamba yupo tayari kufanya mazungumzo iwapo serikali itakuwa tayari kuwaachia huru wanasiasa 11 wanaomuunga mkono ambao walikamatawa wakati vurugu zilipotokea.
Machar aliyasema hayo baada ya serikali kusema ipo tayari kusitisha mapigano makubaliano yaliyopokewa kwa mikono miwili na viongozi wa Afrika Mashariki mjini Nairobi.
Mapigano yaliendelea siku ya ijumaa katika mji wa Makalal, katika jimbo la Upper Nile.
Tayari askari zaidi wa Umoja wa Mataifa wa kuongeza nguvu wamekwishawasili nchini Sudan Kusini.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment