Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, December 25, 2013

Mgogoro nchini Sudani Kusini waendelea kutokota

Aliekua makamo wa rais nchini Sudan Kusin, Riek Machar

Na RFI
Makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini, Riek Machar anasema ataweza tu kuzungumza na rais Salva Kirr hadi pale atakapowaachilia huru wanasiasa wanaouzuiliwa.
Kauli hiyo inakuja wakati, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limepitisha azimio la kuongezwa kwa majeshi ya kulinda amani nchini Sudan Kusini

Hii inaaminisha kuwa idadi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Sudani Kusini itakuwa ni zaidi ya wanajeshi elfu kumi na mbili katika taifa hilo changa linalopitia kipindi kigumu cha machafuko kati ya wanajeshi wa serikali na wale wanaomuunga mkono aliyekuwa Makamu wa rais Riek Machar.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa maelfu ya watu wamepoteza maisha kutokana na mzozo huo na siku ya Jumanne wamegundua uwepo wa makaburi ya pamoja mjini Juba na Bentiu.
Ban ki-Moon amesma licha ya kuongezwa kwa wanajeshi hao haimaanishi kwamba watalinda usalama wa raia wote nchini humo.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 80,000 wamekimbia makwao na wanahifadhiwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Francis M Deng balozi wa Sudan Kusini katika Umoja wa Mataifa, amesema wanaishukuru Jumuiya ya Kimataifa kwa kuendelea kuisaidia Sudan Kusini ili iwe na amani, na kuiomba isichoke.
Rais Salva Kiir amesema wanajeshi wa seriklali wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa mji Mkuu wa jimbo la Joglei wa Bor, huku jimbo la Unity likiendelea kudhibitiwa na waasi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment