Writen by
sadataley
9:03 PM
-
0
Comments
KWA HERI BABA NELSON MANDELA
![]() |
| Nelson Mandela 'Madiba' ©BBC |
Kuna kila aina ya hisia katika taifa la Afrika Kusini mara baada ya kufariki kwa Rais wa kwanza mweusi na mpiganiaji uhuru wa taifa hilo lenye historia ndefu, wakati mishale ya saa ikielekea saa nne usiku, siku ya Alhamisi.
Mandela, mwenye umri wa miaka 95 amekuwa akitibiwa nyumbani kwake kutokana na matatizo ya mapafu, jambo ambalo lilimfanya alazwe kwa muda wa miezi 3 kabla ya kuhamishiwa nyumbani aendelee kutibiwa.
Kona hii watu wanalia, kona nyingine watu wanashangilia, kona nyingine watu wanatafakari namna watakavyoanza kuishi katika ulimwengu huu bila ya Nelson Mandela, kama ambavyo alisema Rais Zuma wakati akitangaza jambo hilo, kwamba, "first sleep in a Mandela-less world", yaani usingizi (usiku) wa kwanza bila ya kuwa na Mandela duniani. Ambapo mida ya saa
Katika mji wa Johannesburg, watu walijikusanya maeneo mbalimbali wakiwa katika hali ya kutoamini kilichotokea, hasa baada ya kupata taarifa kuwa mtetezi huyo aliyetupwa jela kwa miaka 27, alikuja kutoka na kuchukua urais wa nchi hiyo huku akiendelea kupigana dhidi ya udhalimu uliokuwa unaendeshwa na iliyokuwa serikali ya wazungu kipindi hicho.
"Nimefurahi amepumzika, yaani kutaka kuendelea aishi ni uroho, amefanya ya kutosha", alisikika mtu mmoja mitaani humo akisema wakati akiomboleza.
Wengine katika mji wa Soweto, kwenye makazi yake ya zamani ambayo sasa ni makumumbushi, walijikusanya huku wakiimba nyimbo za kuhamasishana kupata ukombozi kama ambavyo zilikuwa zikiimbwa kipindi cha nyuma.
Wengi wataamka wakiwa hawana taarifa, na hivyo kukutana na taarifa hizi wajiandaapo kwa shughuli zao, kutokana na tangazo kutolewa usiku.
"Tulijua siku hii itakuja, lakini bado ni ngumu kwetu." Rais Zuma ananukuliwa akisema kwenye tangazo, akiwa amevalia suti nyeusi.
Kwa upande mwingine, filamu inayohusu maisha ya Madiba, Long Walk to Freedom ilikuwa ikizinduliwa nchini Uingereza kwa mara ya kwanza, na mara baada ya filamu hiyo kumalizika, tangazo lilitolewa kwamba hatunaye tena, jambo lililozua simanzi mara mbili, ya kwanza ikiwa ni ile ya kuangalia ukweli wa mambo kupitia igizo hilo, na ya pili ikiwa ni ile ya kufahamu kwamba uliyemtazama hayupo.
Binti zake wawili, Zindzi na mwenzie ambao walikuwepo kwenye uzinduzi huo, walipewa taarifa kabla na kisha wakaondoka kabla ya onyesho kumalizika, lakini wakawataka kuendelea kuionyesha, kwa waliosalia ukumbini hadi mwisho ndio watangaziwe.
Kiujumla, huu ni msiba wa Afrika, na dunia nzima kwa waliokuwa wanaguswa na matendo ya kiongozi huyu. Gospel Kitaa itakuwa ikikupa maendeleo ya habari hii mara kwa mara, endelea kuwa nasi.

No comments
Post a Comment