Writen by
sadataley
9:04 PM
-
0
Comments
KWA TAARIFA YAKO : JE WAYAJUA AYAWAZAYO CHRISTINA SHUSHO?
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO mdau wetu leo ni kutoka kwa mwanamama Christina Shusho ambaye kama kuna watu wamepewa kibali cha kukubalika na kupendwa na watu basi yeye ni mmoja wapo, mwanamama huyu ambaye amejizolea sifa kemkem ndani na nje ya Tanzania hususani nchini Kenya, album zake zote zimeonekana kupokelewa kwa mwitiko wa hali ya juu sana katika nchi za Afrika mashariki. KWA TAARIFA YAKO kama kuna jambo ambalo mwanamama huyu analiwaza na anataka alitende Mungu atakapompa nafasi basi ni kuanza kuwa shirikisha waimbaji wa muziki wa nje ya kanisa ili washiriki katika matamasha ya injili na kuwashirikisha katika nyimbo zake kabisa.
KWA TAARIFA YAKO wazo hili analo siku nyingi na kwamba wakati anafanya tamasha lake la kwanza katika viwanja vya Leaders Shusho alikuwa amemwalika Ambwene Yessayah (AY) ili kushiriki katika tamasha hilo ila kwabahati mbaya akawa na ratiba nyingine ya kuhudhuria tuzo za channel O nchini Afrika ya kusini. Je unajua kwanini Christina ana wazo hilo?
KWA TAARIFA YAKO ameiambia GK kwamba watu waliopo kanisani wamejisahau sana kuhusu kuwaalika na kuwahubiria watu ambao inaonekana wapo nje na neno la Mungu lakini watu hao watajuaje neno ama kumkaribia Mungu endapo hakuna mtu anayewapa mwaliko wa kwenda kanisani ama kushiriki katika matamasha ya injili. "Watu waliopo kanisani tayari wamelisikia neno na bado wanaendelea kulishwa na neno, sasa ni wakati wa sisi tunaoitwa walokole ama watu wa Mungu kwenda mitaani kuwavuta na wengine ili kuona maisha tunayoishi ili wajifunze kwayo na pengine upo uwezekano mkubwa wa wao kubadilika na kumrudia Mungu". alisema Shusho.
KWA TAARIFA YAKO Christina bado anampango huo wakuwavuta watu wengi zaidi kwa Yesu kwakuwaalika ili wahudhurie mikutano ya dini na mikutaniko yoyote inayomwinua Kristo. Christina ambaye ameachia video ya Nataka Nimjue mapema mwezi September mwaka huu amekuwa akipata mialiko sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi ambako ameendelea kujifunza mengi ambayo watu wa Mungu wa nchi hizo wanafanya ili kuwahubiria neno watu walioko nje ya kanisa.
Katika kuonyesha kwamba zoezi hilo linaweza kuzaa matunda yupo mwimbaji wa muziki wa kufokafoka nchini Kala Jeremiah ambaye katika mahojiano na kipindi cha Chomoza Clouds Tv alisema wazi anatamani sana kuimba katika jukwaa moja na waimbaji wa nyimbo za injili tatizo hawapewi mwaliko.

Habari na Gospel Kitaa

No comments
Post a Comment