Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, October 3, 2013

Mkutano wa vijana kufanyika SA

Kile kinachosemekana kuwa mkutano mkubwa zaidi wa vijana unatarajiwa kuanza hivi punde mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Vijana nchini Afrika Kusini wakiadhimisha siku ya vijana duniani
Vijana efu moja miatatu kutoka katika mataifa ya 93, watahudhuria kongamano hilo liitwalo, dunia ya vijana katika uwanja rasmi wa michezo mjini humo.
Mkutano huu wa siku 4 utawajumuisha vijana 1300 chini ya umri wa miaka 30 kutokea mataifa 180 na mada kuu ni vijana kujifundisha utawala bora na kuwa viongozi wa kesho,ilimu ,haki za Binadamu, ukosefu wa ajira miongoni mwa mambo mangine mengi.Watajadili maswala kama vile ajira kwa vijana, elimu na dhuluma za kingono.
Wengi ya vijana wanaume kwa wanawake wanaotarajiwa kuhudhuria kongamano hili ni vijana wanaotokea katika mataifa yaliokumbwa na misukosuko ya kivita lakini vijana wa vyama tawala kutoka serekali za mataifa hayo 180 hawakualikwa ilivyokua kongamano hili sio kongamano la kiserikali.
Baadhi ya vijana wanaotarajiwa kushiriki kwenye mkutano huu wa mara ya nne wa One Young World ni Kevin Musila na Billow Hassan kutokea Kenya , Arinitwe Stephen kutokea Uganda na Ilwad Elman kutokea Somalia.
Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, msanii wa muziki wa Rock, Bob Geldoff na mshindi wa tuzo ya Nobel kutoka Bangladesh Mohammad Yunis, ni miongoni mwa watakaowahutubia vijana hao
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment