Writen by
sadataley
11:40 PM
-
0
Comments
Balozi wa Umoja wa Mataifa UN nchini Mali, Bert Koenders amehimiza kundi la wapiganaji la Tuareg na waasi wa kiarabu kurejea katika mazungumzo ya amani na serikali ya Mali ili kuhitimisha mzozo unaondelea kutatiza usalama wa Kaskazini mwa nchi hiyo.
Katika mazungumzo yake na Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore, Koenders ametoa mfano wa mapigano yaliyoshuhudiwa hivi karibuni na kuyasihi makundi hayo kushiriki katika mazungumzo na serikali ya Bamako ili kurejesha usalama wa Taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.
Mwishoni mwa mwezi Septemba, waasi hao walitangaza kujitoa kwenye mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakiendelea kati yao na serikali ya Rais mpya wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keita.
Mwishoni mwa mwezi Septemba, waasi hao walitangaza kujitoa kwenye mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakiendelea kati yao na serikali ya Rais mpya wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keita.
Siku moja baada ya uamuzi huo kutolewa mapigano mapya yalizuka eneo la Kaskazini mjini Kidal ambapo wanajeshi wawili wa serikali walijeruhiwa katika shambulio la guruneti.
Kwa mujibu wa serikali ya Bamako, shambulio hilo lilifuatiwa na na jingine mjini Timbuktu ambapo wananchi wawili waliuawa na wanajeshi sita kujeruhiwa.

No comments
Post a Comment