Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, October 8, 2013

Idadi ya wahamiaji haramu waliopoteza maisha kisiwani Lampedusa yafikia 194

Juhudi za uokozi katika kisiwa cha Lampedusa
Na Victor Melkizedeck Abuso

Wapigambizi nchini Italia wameendelea kutafuta miili zaidi ya wahamiaji haramu kutoka barani Afrika waliozama na kuangamia  katika kisiwa cha Lampedusa wiki iliyopita.
Waokoaji hao wanasema kuwa tayari wamefanikiwa kupata miili 83 zaidi  kufikia siku ya Jumapili juma lililopita.
Hadi sasa idadi ya watu waliopteza maisha yao kutokana na mkasa huo imefikia 194 na wengine 200 bado hawajulikani waliko.
Hata hivyo, wahamiaji haramu 155 waliokolewa baada ya boti yao kuzama kwa kile wataalam wanasema kuwa chanzo kilikuwa ni kushika moto kwa mitambo ya boti hiyo iliyokuwa na wahamiaji haramu 500 wakitokea nchini Somalia na Eritrea.
Serikali ya Italia imekanusha madai kuwa imekuwa ikifanya uokoaji tarabatibu na tayari serikali ya Ufaransa imetaka kufanyika kwa kikao cha dharura cha Umoja wa Ulaya kujadili suala la ongezeko la wahamiaji haramu wanaokimbilia barani humo.
Serikali ya Italia, imesema kuwa itarekebisha sheria za uhamiaji ili kukabiliana na kuingia kwa wahamiaji haramu nchini humo kutokana na idadi yao kuongeza katika siku za hivi karibuni.
Mamia ya wahamiaji haramu hukimbilia barani Ulaya kwenda kutafuta maisha mazuri kutokana na hali ngumu ya maisha ya usalama katika nchi zao.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment