Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, October 2, 2013

ICC yataka kukamatwa mwandishi habari Kenya.

Mwendesha mashataka mkuu wa ICC Fatou Bensouda.
Mwendesha mashataka mkuu wa ICC Fatou Bensouda.
Mahakama ya uhalifu ya kimataifa imetoa kibali cha kukamatwa kwa mwandishi habari wa zamani anayeshutumiwa kwa kutoa hongo kwa mashahidi katika kesi ya naibu rais William Ruto .

Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda alitangaza jumane kwamba Kenya ilipata kibali cha kumkamata haraka Walter Barasa na kumpeleka katika mahakama ya ICC mjini Hague.

Katika taarifa iliyorekodiwa Bensouda alisema Barasa alishiriki katika kuingilia mashahidi kwenye kesi inayomkabili naibu rais  wa Kenya.

Anasema ushahidi uliokusanywa hadi Sasa unaonesha kuna mtandao wa watu ambao wanajaribu kuvuruga kesi ya Ruto kwa kuingilia mashahidi upande wa mashtaka ambapo Barasa ni mmoja wao.

Amesema kutolewa kibali hicho cha kukamatwa itakuwa onyo kwa wengine. Kama atakutwa na hatia barasa anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Amri ya kukamatwa ilitolewa Jumatano  wakati naibu rais Ruto anakwenda ICC kushiriki kuanza tena kusikilizwa kesi yake. Yeye na rais Uhuru Kenyatta wanashitakiwa katika kesi tofauti za uchochezi wa ghasia za mauaji baada ya uchaguzi wa rais mwaka 2007.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment