Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, September 19, 2013

Wapinzani wataka watanzania kujadili sheria ya mabadiliko ya katiba

Bunge la Tanzania
Bunge la Tanzania
Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Tanzania  wamesisitiza madai yao ya kutaka kurejeshwa bungeni muswada wa sheria ya  mabadiliko ya katiba ili kuendelea na mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya yenye ridhaa ya watanzania wote.

Wakizungumza katika mahojiano maalum na sauti ya Amerika-VOA  viongozi hao Freeman Mbowe wa CHADEMA, James Mbatia wa NCCR MAGEUZI na Profesa Ibrahim  Lipumba wa CUF wamesema kilichofanyika bungeni kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi-CCM kupitisha muswada huo wa sheria ya mabadiliko ya katiba kibabe kutaliweka taifa  katika wakati mgumu kupata katiba bora yenye maslahi kwa watanzania wote.
Wapinzani walisusia mjadala wa sheria ya mabadiliko ya katiba bungeni hivi karibuni wakiwa na madai kadhaa kubwa zaidi ni kutoshirikishwa wananchi wa upande wa Zanzibar, vipengele vya muswada huo vinavyompa madaraka makubwa Rais wakati wa upatikanaji wa wajumbe wa bunge maalum la katiba na pia kipengele kinachoivunja tume ya mabadiliko ya katiba mara tu tume hiyo inapokabidhi rasimu kwenye bunge la katiba.

Viongozi hao wa vyama vya upinzani Jumanne walikutana na wajumbe wa jukwaa la katiba na asasi nyingine zisizo za kiserikali ikiwa ni harakati za kuunganisha nguvu kupinga muswada huo ambao unasubiri saini ya Rais ili kuwa sheria.

Aidha vyama hivyo vya CHADEMA, NCCR MAGEUZI na CUF vimeandaa mikutano ya hadhara wakianzia jijini Dar Es Salaam, Zanzibar,  Mwanza, Arusha, na Kigoma ili kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kwamba mchakato wa mabadiliko ya katiba kwa sasa hauko sawa  na hivyo wanapaswa kushinikiza mabadiliko yenye tija kwa taifa zima.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment