Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, September 18, 2013

Ufaransa yalalamikia mauaji ya raia wake Misri

Serikali ya Ufaransa inasema kuwa raia wake mmoja amefariki akiwa amezuiliwa na polisi mjini Cairo.
Polisi wa Misri walikuwa na kibarua kigumu kukabiliana na waandamanaji wakati Morsi alipoondolewa mamlakani
Duru za usalama nchini humo zimesema kuwa mtu huyo alichapwa na watu aliokuwa amezuiliwa nao hadi kufariki katika kituo kimoja cha polisi.
Mtu huyo inaarifiwa alikamatwa baada ya kukiuka agizo la kutotoka nje usiku kucha.
Agizo hilo limewekwa kama sehemu ya sheria ya hali ya hatari, iliyowekwa na serikali ya kijeshi kutokana na mgogoro uliozuka baada ya Mohammed Morsi kuondolewa mamlakani na jeshi.
Ubalozi wa Ufaransa unasema kuwa unatafuta taarifa zaidi kuhusu tukio hilo na hasa kilichosababisha kifo cha raia huyo wa raia wake ambaye alikuwa ameishi Misri kwa muda mrefu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment