Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, September 19, 2013

Polisi Afrika.K matatani kwa kudanganya

Polisi wa Afrika Kusini wanatuhumiwa kwa kudanganya kuhusu mauaji ya Marikana yaliyotokea mwaka jana, ambapo wachimba migodi 34 waliuawa. Taarifa hii ni kwa mujibu wa tume ya uchunguzi iliyokabidhiwa jukumu la kuchunguza mauaji hayo.

Wachimba migodi wa Marikana waliandamana wakidai nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi
Inasemekana polisi walitoa ushahidi wa uongo au kuficha nyaraka ambazo zilitoa taarifa za uongo kuhusu matukio katika mgodi huo.
Kitendo cha polisi kuwauawa kwa kuwapiga risasi wachimba migodi katika mgodi unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin kiliwashtua sana wengi nchini humo.
Polisi walisema kuwa walikuwa wanajikinga kutokana na kuvamiwa na wachimba migodi hao siku chache baada waandamanaji kudaiwa kuwanyonga polisi wawili.
Tume ihiyo iliteuliwa na Rais Jacob Zuma kuchungza mauaji hayo ambayo yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kufanywa na polisi tangu kukamilika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi.
Taarifa yake ambayo imekuja siku kumi baada ya kupata taarifa za polisi kwenye komputa zao na pia kupitia nyaraka zao.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment