Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, September 20, 2013

Lipumba, Mbowe, Mbatia wapigwa stop


Ni maandamano ya kesho
Polisi wadai wamepata taarifa za kiinterijensia
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limezuia maandamano yaliyopangwa kufanywa kesho na vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kwa lengo la kupinga mchakato wa Katiba mpya.

Maandamano hayo pia yana lengo la kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete asiusaini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa madai kuwa umehodhiwa na Chama Cha Mapindizi (CCM).

Hata hivyo, polisi imeruhusu vyama hivyo kufanyika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Jangwani kesho lakini havitaruhusiwa kufanya maandamano.

Maandamano hayo ambayo yangewashirikisha viongozi, wanachama na wafuasi wa vyama hivyo, yalipangwa kuanzia eneo la Tazara Veterani kupitia Barabara ya Mandela hadi Buguruni Sheli, Uhuru kupitia Malapa, Karume, mzunguko wa Shule ya Msingi Uhuru, Msimbazi, Fire Barabara ya Morogoro hadi viwanja vya Jangwani.

Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema Jeshi la Polisi halioni umuhimu na sababu za msingi za kufanya maandamano hayo kwani kuna uwezekano mkubwa wa kutokea uvunjifu wa amani.

Kamishna Kova alisema sehemu ambazo maandamano hayo yalipangwa kupita kuna mkusanyiko mkubwa wa watu ambao watakuwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, usafirishaji na mahitaji mengine ya kila siku ya kibinadamu.

Aidha, Kamishna Kova alisema Jeshi la Polisi limepata taarifa za kiintelijensia kuwa vyama hivyo vimeandaa  uhamasishaji mkubwa kwa watakaotumia pikipiki, guta na watembea kwa miguu.

Kabla ya Kova kutoa uamuzi huo, alikutana katika kikao cha ndani na viongozi wa vyama hivyo.

Katika mkutano huo, CUF kiliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Julius Mtatiro na Hamidu Bobali wakati Chadema kiliwakilishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), John Heche na  Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo, Singo Benson.  Hata hivyo, NCCR-Mageuzi hakikuwakilishwa na kiongozi yeyote.

Kamishna Kova alisema vyama hivyo vikifanya mkutano kwenye viwanja hivyo inatosha kupeleka ujumbe kwa wananchi na maudhui katika kusudio la la kuwashirikisha wananchi katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya.
Alisema kama vyama hivyo havijaridhika na makubaliano ya mkutano waliokaa kwa zaidi ya saa mbili na kuafikiana kusitisha maandamano hayo waende kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, ambaye ndiye atatoa maamuzi zaidi.

“Jeshi letu limejipanga kupeleka askari wa kutosha na katika viwanja hivyo kwa ajili ya usalama zaidi na iwapo kutakuwa na mabadiliko kutoka ngazi za juu, sisi tutatii,” 
alisema Kamishna Kova.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment