Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, September 3, 2013

Ligi ya Uingereza yavunja rekodi


Mkufunzio wa Arsenal Arsene Wenger
Vilabu vya ligi kuu ya Uingereza vimetumia pauni milioni 630 katika kipindi kilichokamilika cha kuwasajili wachezaji wapya kutoka vilabu vingine, kulingana na kitengo kinachohusika na maswala ya biashara ya michezo katika kampuni ya Deloitte.
Rekodi ya awali ilikuwa pauni milioni 500 iliyowekwa mwaka 2008. Kipindi cha wachezaji kuruhusiwa kuhama kutoka vilabu fulani na kusajiliwa kwengineko, kilifika kikomo hapo jana siku ya Jumatatu
Miongoni mwa wachezaji waliogharimu mamilioni ya pauni ni mchezaji Mesut Ozil aliyehama kutoka Real Madrid na kuelekea Arsenal kwa kima cha pauni milioni 42.4.
Mesut Ozil
                                                               Mesut Ozil wa Ujerumani
Manchester United ilimsajili Marouane Fellaini kwa pauni milioni 27.5 kutoka Everton.
"kisa cha msimu huu wa wachezaji kuhama ni kuwa rekodi imevunjwa , msimu huu mamilioni imetumiwa kuliko katika msimu mwingine wowote katika historia ya Ligi ya Uingereza,'' alisema Dan Jones wa Deloitte.
Hata hivyo mchezaji Gareth Bale, alihamia Real Madrid kutoka Tottenham Hotspur kwa kima cha pauni milioni 85.
Gareth Bale
                                                                                      Gareth Bale
Vilabu hivyo sasa viko na pesa nyingi sana kutokana na mikataba iliyotiwa saini kati ya vilabu ya televisheni za uingereza kupeperusha mechi zao.
Mfano BT imelipa pauni milioni 738 kwa kipindi cha miaka mitatu kuweza kupeperusha mechi moja kwa moja kutoka viwanjani wakati televisheini ya Sky ikilipa pauni bilioni 2.3 kupeperusha mechi 116 msimu huu.
Ingawa ligi zengine ulaya hazijfikia utumaiji wa pesa kwenye ligi ya Uingereza, zimetumia mamilioni katika kuwanunua wachezaji kutoka vilabu vingine
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment