Writen by
sadataley
7:21 AM
-
0
Comments
Na Ahmed Makongo
Bunda. Diwani wa Kata ya Kisorya wilayani hapa, Misana Jigwira (CCM), amesema yuko tayari kuachia nafasi yake kwa kujiuzulu, iwapo mganga mkuu mfawidhi wa kituo cha afya cha kata hiyo hatahamishwa kazi.
Jigwira alisema atachukua hatua hiyo kutokana na mganga huyo, kutokuwajibika ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kutokuwapatia dawa wagonjwa wanaofika kituoni hapo licha ya kuchangia fedha papo kwa papo kiasi cha Sh1,000 kwa kila mgonjwa na kwamba kwa sasa fedha hizo zimeongezeka na kufikia Sh3,000.
Diwani huyo bila kutafuna maneno alisema licha ya wagonjwa hao kuchangia fedha hizo, huambiwa na mganga huyo kwamba dawa hazipo na kuwaagiza waende kununua kwenye maduka ya watu binafsi.
Alisema kutokana na kero hiyo wananchi wamekuwa wakifika kwake mara kwa mara kulalamikia hali hiyo, ikiwa ni pamoja na huduma duni wanazopata kwenye kituo hicho.
Chanzo:http://www.mwananchi.co.tz
No comments
Post a Comment