Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, August 9, 2013

ULIPAJI WA ADA ZA MAGARI KWA MTANDAO KUANZA LEO.


Akizungmza na gazeti hili jana, Meneja Mahesabu na Makusanyo ya Serikali katika mamlaka hiyo, Ramadhan Sengati alisema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 37 ya ongezeko la mapato hayo.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inatarajia kuvuna kiasi cha Sh217.8 bilioni kwa mwaka, baada ya kuanzishwa kwa mfumo mpya wa kulipa ada za magari kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi na benki, unaoanza leo.
Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, mamlaka hiyo ilikuwa na uwezo wa kukusanya kiasi cha Sh147 bilioni kwa mwaka.
Akizungmza na gazeti hili jana, Meneja Mahesabu na Makusanyo ya Serikali katika mamlaka hiyo, Ramadhan Sengati alisema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 37 ya ongezeko la mapato hayo.
Sengati alisema kiasi hicho ni mara mbili ya makusanyo yaliyokuwa yakikusanywa kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo mpya.
Alisema hatua hiyo inatokana na maboresho ya mifumo ya kielektroniki ambayo TRA inaendelea kuyafanya ikiwa ni juhudi za kutoa huduma bora kwa walipakodi.
“Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali yanakusanywa na yanawasilishwa kwa wakati kwenye mfumo mkuu wa Serikali na benki kuu na kwamba kwa sasa TRA itakuwa inakusanya Sh217.8 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 37 kutoka Sh147 bilioni zilizokuwa zikikusanywa hapo awali kabla ya kuwepo mfumo huu,” alisema.
Wiki iliyopita TRA ilitangaza kuanzisha mfumo huo kwa lengo la kupunguza msongamano na wizi unaofanya na vishoka.
Kuanzishwa kwa mfumo huo ni sehemu ya jitihada za kutoa huduma bora kwa walipakodi na kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali yanawasilishwa kwa wakati.
Mkurugenzi wa Huduma na elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Richard Kayombo alisema mfumo huu utasaidia kumpatia taarifa ya kiasi cha kodi anachotaka kulipa mteja.

Habari kutoka Gazeti la mwananchi
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment