Writen by
sadataley
9:34 AM
-
0
Comments
![]() |
| Askofu Tutu katika kampeni ya kupigania usawa kwa wapenzi wa jinsia moja. ©AFP/Getty Images |
Kama ni siku za mwisho basi ni hzi, maana kauli tata kutoka kwa viongozi wa juu wanaoheshimiwa nazo zinaonekana kuzidi kushamiri. Na hivi sasa ni kutoka kwa Askofu mkuu mstaafu wa kanisa la Anglikan nchini Afrika Kusini, Desmond Tutu, ambaye amenukuliwa akitetea mashoga na kusema kwamba kama mbingu inawatenga mashoga, basi ni nafuu kwake asiende mbingu hiyo.
“I would not worship a God who is homophobic, and that is how deep I feel about this,” Tutu said at a United Nations’ gay rights campaign function in Cape Town, South Africa. “I would refuse to go to a homophobic heaven. 'No,' I would say. 'Sorry. I mean, I would much rather go to the other place.'”
Sitamuabudu Mungu ambaye hapendezwi na ushoga (mapenzi ya jinsia moja) na hiyo ndio namna ninavyosikia kuhusu jambo hili. Tutu alisema katika kampeni ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za mashoga jijini Cape Town, Afrika Kusini. Nitakataa kwenda kwenye mbingu inayokataa mashoga. 'Hapana,' Nitasema, 'Samahani, yaani nafuu niende ule upande mwingine.
NI nukuu ya askofu Tutu ambaye alienda mbele zaidi na kufananisha harakati za kutetea haki za ndoa za jinsia moja sawa na haki ya watu weusi wakati wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Ninaguswa na kampeni hii kama ambavyo niliguswa na kampeni dhidi ya ubaguzi wa rangi. Alinukuliwa Tutu na shirika la habari la Ufaransa. AFP.
Kufuatia kauli hiyo aliyoitoa mnamo mwisho wa mwezi Julai, askofu mkuu wa Anglikan nchini Ghana, Yinkah Sarfo amelaani kauli ya Tutu na kusema kuwa huenda askofu huyo alihongwa pesa na wanaharakati wa ushoga ili aseme hivyo.
Habari na Gospel Kitaa

No comments
Post a Comment