Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, August 16, 2013

Sheikh Ponda apelekwa gerezani

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia)akiwa ndani ya gari la Polisi baada ya kutolewa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), kupelekwa gerezani, Dar es Salaam jana
Dar es Salaam. Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba na Mifupa (Moi), jana aliondolewa na kupelekwa katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam. Kitendo hicho kimelaaniwa vikali na familia yake na wafuasi wake, ambao wamepanga kufanya maandamano makubwa leo
Sheikh Ponda, ambaye alisomewa shtaka la uchochezi akiwa kitandani na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka ilidaiwa kuwa alitenda kosa hilo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Juni 2 mpaka Agosti 11, mwaka huu.
Alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hellen Liwa.
Jana, Polisi waliimarisha doria kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia saa 1:30 asubuhi. Magari matatu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia(FFU) yaliyobeba askari wenye silaha yalionekana yakiranda katika maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
Sheikh Ponda alitolewa wodini saa 4:20 asubuhi chini ya ulinzi mkali wa askari baadhi yao wakiwa wamebeba silaha.
Alionekana akiwa ameshikiliwa na polisi kutokana na kukosa nguvu ya kutembea.
Akiwa amevalia shati lenye rangi ya udongo, kikoi cheupe na kandambili, Sheikh Ponda alipakiwa kwenye gari ndogo aina ya Landcruiser nyeupe lililokuwa na vioo vya giza.
Baada ya kupakiwa, safari ya kuelekea Segerea ilianza saa 4:45. Gari lililombeba lilitanguliwa na gari la FFU lililokuwa na askari wenye silaha likifuatiwa na magari mengine mawili ya FFU yaliyokuwa na polisi wenye sare na magari mengine mawili ambayo yalikuwa na askari kanzu.

Wakili ashangaa, familia yaja juu
Akizungumza baada ya tukio hilo jana, Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro alisema hakuwa na taarifa za kuondolewa hospitali kwa mteja wake na kueleza kushangazwa na kitendo hicho akisema mteja wake alikuwa mgonjwa akiwa anahisi maumivu makali ya kidonda tangu juzi.
“Nimepigiwa simu mchana huu na mmoja wa wanafamilia, nimeshangaa sana kwa sababu nakumbuka jana (juzi Jumatano) Sheikh alishindwa kufanyiwa mahojiano na polisi kutokana na kuhisi maumivu na kizunguzungu,” alisema Nassoro.
Picha na Venance Nestory 
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment