Writen by
sadataley
10:20 AM
-
0
Comments
“Ninawapongeza Kanagisa na Nanai kwa kujiunga na Timu ya MCL, kikubwa ni kwamba tuwape ushirikiano katika majukumu yao mapya.” Tido Mhando
Dar es Salaam. Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), imeunda nafasi mbili za juu za utawala kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake.
Dar es Salaam. Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), imeunda nafasi mbili za juu za utawala kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Tido Mhando ilieleza kuwa Francis Nanai ameteuliwa kuwa Ofisa Uendeshaji Mkuu wa MCL
Mhando alisema Emmanuel Kanagisa ameteuliwa kuwa Meneja Mkuu Usambazaji.
Nyadhifa zote mbili ni mpya kwenye muundo wa uongozi wa MCL inayochapisha Magazeti yaMwananchi, Mwananchi Jumamosi,Mwananchi Jumapili,Mwanaspoti, The CitizenOn Saturday na The Citizen On Sunday. Nanai alianza kutekeleza majukumu yake Agosti Mosi, mwaka huu wakati uteuzi wa Kanagisa kushika nafasi hiyo ulianza Julai Mosi.
“Ninawapongeza Kanagisa na Nanai kwa kujiunga na Timu ya MCL, kikubwa ni kwamba tuwape ushirikiano katika majukumu yao mapya,” alisema Mhando.
Akizungumza baada ya kukaribishwa, Nanai alisema atashirikiana na watendaji mbalimbali kuhakikisha wafanyakazi wa MCL wanafanya kazi kwa ufanisi na kujituma.
“Hatuweza kufanya kazi kwa mazoea, lazima tubadilike, na kwa Kampuni yetu kuwa namba moja, lazima kufanya kazi kwa bidii na ufanisi,’’ alisema Nanai mwenye Shahada ya Uchumi na Shahada ya Uzamili za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Utawala wa Biashara-Uchumi akijikita katika masoko.
Alisema kuwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma, kutasaidia kukata kiu ya kila Mtanzania hasa katika kupata huduma za MCL kwa wakati.
Kabla ya kujiunga na MCL, Nanai aliwahi kufanya kazi katika Kampuni za; Lafarge Tanzania, Kampuni ya Saruji Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara zaidi katika masoko, mauzo na mipango.
Pia alifanya kazi kwenye Kampuni ya Coca-Cola Kwanza akiwa Mkurugenzi wa Masoko na kimsingi ni mzoefu wa masuala ya mipango ya maendeleo ya biashara na masoko.
Kanagisa mwenye Shahada ya Masoko ya UDSM na Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara kwa Biashara ya Kimataifa aliyoipata katika Taasisi ya Biashara ya Nje India, atakuwa na kazi ya kuhakikisha magazeti yanayotolewa na MCL yanamfikia kila Mtanzania.
“Tunataka kuanza kuuza magazeti kwa Dar es Salaam kuanzia saa 6:00 usiku kila siku na mikoani yatakuwa ubaoni kuanzia saa 2.00 asubuhi,’’ alisema.
MCL imepiga hatua za mafanikio hasa baada ya kuanzishwa kwa nafasi mbalimbali ikiwamo Kitengo cha Maendeleo ya Biashara kinachoongozwa na Theophil Makunga.
Makunga alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa kitengo chake, kampuni imepanua wigo wa biashara ndani na nje ya nchi na kwamba lengo ni kuendelea kukua zaidi na kuwafikia Watanzania wote.
Chanzo:http://www.mwananchi.co.tz
No comments
Post a Comment