Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, August 17, 2013

Mauaji Kenya : Alshabaab yawaua polisi 4

Wanamgambo wa kisomali wamewauawa kwa kuwapiga risasi polisi wanne wa Kenya karibu na mpaka wa Somalia, maafisa wamesema.
Mji wa Garissa : Mpaka wa Kenya na Somalia
Takriban watu 40 waliojihami kwa silaha walishambulia kituo cha polisi Ijumaa jioni, kamishna wa kaunti hiyo amesema.
Kundi la alshabaab limethibitisha kufanya shambulio hilo.
Kenya imekumbwa na msururu wa mashambulio tangu majeshi yake yaingie kusini mwa Somalia kukabili wapiganaji wa Alshabaab mwaka wa 2011.
Kamishna wa Kaunti hiyo Rashid Khattor ameambia wanahabari : "maafisa wanne wa polisi wameuawakatika shambulio hilo na tunajiandaa kusafirisha miili yao kutoka eneo hilo.
Eneo hilo karibu na Garissa limekuwa likipata mashambulio ya mara kwa mara katika miezi chache iliyopita. Watu 8 waliuawa katika shambulio mwezi Aprili na wengine watano mnamo mwezi Januari.
Imewekwa na Happy Adam
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment