Writen by
sadataley
11:33 AM
-
0
Comments
Moshi. Waziri wa Wizara ya Maji, Profesa Jumanne Maghembe amewaagiza watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Taka mjini Moshi (MUWSA), kutopeleka masuala yanayohusu mamlaka hiyo kwenye Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) ama polisi kwani kwa kufanya hivyo wanasababisha migogoro isiyo ya lazima.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi, Maghembe alisema ni vyema wakapeleka matatizo yao kwenye bodi na iwapo hawataridhika na utatuzi wake wapeleke kwenye Chama cha Wafanyakazi (TUICO) au kwa Waziri mwenye dhamana kwa kuwa kushtakiana kunarejesha nyuma utendaji kazi wa mamlaka hiyo.
Waziri Maghembe alisema ni vyema wakajenga utamaduni wa kumaliza matatizo yao kwa kutumia vikao na siyo kushtakiana kwa mambo yasiyo ya msingi ambayo mwishowe yanaleta migogoro na kurudisha nyuma utendaji kwazi wa mamlaka.
Katika hatua nyingine Waziri Maghembe aliiagiza Ofisi ya Bonde la maji Pangani kusitisha uchimbaji wa visima kwa wawekezaji ama wafanyabiashara wanaotaka kumiliki visima vya maji maeneo ambayo mamlaka ya maji ina uwezo wa kufikisha huduma hiyo.
Alisema MUWASA imepewa kibali cha kusambaza maji mjini Moshi hivyo ni vyema wanaotaka kuchimba visima wakachimbiwa na mamlaka husika.
Waziri alilazimika kutoa agizo hilo kutokana na malalamiko ya wafanyakazi waliolalamikia uchimbaji wa visima unaofanywa na wawekezaji wa kahawa.
chemichemi ya Nsere hali iliyosababisha kupungua kwa maji katika chanzo hicho.
No comments
Post a Comment