Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, August 30, 2013

MAOMBOLEZO YA MSIBA WA ASKOFU DKT MOSES KULOLA YAENDELEA

Sehemu ya watu waliofika jioni kwenye msiba, EAGT Temeke.
Hatimaye ratiba kuhusu maazishi ya aliyekuwa askofu mkuu wa makanisa ya Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Moses Kulola, imetoka na inaonyesha kuwa maazishi yatafanyika Mwanza siku ya Jumatano Septemba 4 kwenye kanisa la EAGT Bugando.

Akitoa taarifa hiyo eneo ambapo msiba umewekwa, EAGT Temeke, katibu wa EAGT kanda ya Mashariki Kusini, Askofu Alphonse Mwanjala ameeleza kuwa kutakuwa na ibada za maombolezo hadi Ijumaa na kwa siku ya Jumamosi mwili utawasili Temeke kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tisa mchana ambapo utaagwa na hatimaye kupelekwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nyerere kwa ajili ya kuusafirisha siku ya Jumapili kuelekea Mwanza.

Na huko Mwanza pia taratibu nyingine zitafanyika na hatimaye mwili kupumzishwa siku ya Jumatano EAGT Bugando.

Christ Gospel Messengers watakuwepo Temeke na kufanya mkesha kwa siku zote hadi mwili utakaposafirishwa. 

Askofu David Mwasota, katibu mkuu wa baraza la makanisa
ya Kipentekoste Tanzania (PCT).
Kwa upande mwingine Katibu Mkuu wa baraza la makanisa ya Kipentekoste (PCT) nchini, Askofu David Mwasota, anasikitika kutangaza kifo hicho na kuwataka wachungaji, maaskofu, mitume, manabii na walimu wote kukutana siku ya kesho kwanye kanisa la mito ya Baraka kwa Askofu Bruno Mwakibolwa ili kufanikisha zoezi zima la kumpumzisha Askofu Kulola atakesafirishwa kwenda Mwanza.

Katika mahojiano na Gospel Kitaa, Askofu Mwasota ambaye pia ni mtoto wa kiroho wa Askofu Kulola,
Habari na Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment