Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, August 13, 2013

KIONGOZI WA WAFANYA BIASHARA AUAWA AFRIKA KUSINI

Afisaa mmoja wa chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa migodini (NUM) ameuawa kwa kupigwa risasi katika mgodi wa madini wa Marikana nchini Afrika Kusini ambako wachimba migodi wengine 34 waliuawa na polisi mwaka mmoja uliopita.
Wachimba migodi 34 waliuawa mwaka jana katika mgodi wa Marikana
Wanachama wenzake wamesema kuwa mwanamke huyo ambaye ni muuza duka aliuawa asubuhi ya leo.
Uhasama kati ya vyama vya wafanyakazi, katika mgodi huo umesababisha kuuawa kwa wafanyakazi kadhaa katika mwaka mmoja uliopita.Wanachama wa chama cha (NUM) wametaja mauaji hayo kama mabaya sana na kusema kuwa wameghadhabishwa mno..
Haijulikani ikiwa mauaji ya leo yanahusishwa na mzozo uliopo sasa kati ya vyama hasimu vya wafanyakazi.
Chama cha NUM kimesema kuwa kimekasirishwa na polisi kutopiga hatua katika kuwakamata wahusika kwa kile walichosema ni mauaji ya kupangwa katika mgodi wa Marikana.
Msemaji wa Lonmin, Sue Vey, aliambia shirika la Reuters kuwa polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza mauaji hayo.
Mauaji yaliyotokea mwaka jana mwezi Agosti yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu Afrika Kusini kupata uhuru.
Imewekwa na Happy Adam
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment