Writen by
sadataley
9:13 PM
-
0
Comments
| Mtoto akiwa bize na mama yake (picha hii haina uhusiano na mtoto aliyeandikwa kwenye habari.) ©Dreamstime |
Jaji Lu Ann Ballew ambaye amesema kuwa mtoto huyo atapata shida kutoka kwenye jamii ya watu wa eneo analoishi na kwamba mtoto huenda asingekubali kutokana na shida ambazo atapata mtaani kutokana na kuchaguliwa jina, amepingwa na mama mzazi wa mtoto huyo mwenye umri wa miezi 7, ambaye amepewa jina la Messiah DeShaw Martin.
"Messiah ni cheo, na kimepatikana kwa mtu mmoja tu, na huyo mtu ni Yesu Kristo." Jaji Ballew alikiambia kituo cha habari cha WBIR.
Chanzo cha dhahama hiyo kama ambavyo inaonekana kwa mama wa mtoto huyo, ni pale ambapo wazazi (yeye na mumewe) walishindwa kukubaliana kuhusu jina la mwisho la kumpa mtoto, na hatimaye kwenda kwenye mahakama ya malezi ya mtoto ambapo Jaji akaja na uamuzi wake.
Hata hivyo mama wa mtoto huyo amesema kuwa atakata rufaa kutokana na maamuzi ya jaji huyo, kwani hayajamridhisha hata kidogo na kwamba hakuyategemea.
Chanzo: Blog ya Gospel kitaa
No comments
Post a Comment