Writen by
sadataley
6:48 PM
-
0
Comments
Baba Askofu Dkt. Owdenburg Moses Mdegella akizungumza na Waandidshi wa Habari
Hapa alipokuwa akitoa ufafanuzi wa muundo na namna aonavyo Serikali zinavyoweza shirikianaWaandidshi wa Habari
Baaadhi ya Waandidshi wa Habari
Hayo ameyasema leo hii alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa. Baba Askofu alikuwa akizungumza juu ya Katiba na Muungano. Alitoa makzo kuwa viongozi wetu wote wamejilimbikizia mali hivyo tofauti kati ya masikini na matajiri ni kubwa sana. Akizungumzia juu ya Uraia wa Muungano alikubaliana nao kwani unatokana na kuzaliwa mahali husika. Kumbe vitambulisho vyetu vya uraia vitaandikwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hapa sasa tunazungumzia raia wa nchi moja na si vinginevyo. Hebu tutazame maoni ya wanaotaka serikali moja, mbili na tatu na kisha walete yale maoni kwa maana ya mtazamo wetu wa kimaongozi kama ni serikali tatu,mbili au moja.
Hivi kweli kuna ndoa inayoruhusu kugawana vyumba, huo ni udanganyifu. Hivyo sura ya 6-7 za rasimu ya katiba hadi aya ya 84 hivi zinapaswa kubadilika.
Tunapaswa kuwa na serikali mbili aua moja tu , tuzingatie hali ya wananchi wa kawaida na si uchama au ushabiki fulani. Hivi hii serikali ya tatu itatawala vipi na makao yake yatakuwa wapi?Hivi kweli mtu wa kawaida wa kijijini anataka serikali tatu yeye anataka apate soko la mazao yake tu.
1Samweli 8:4-18(OMBI LA KUPEWA MFALME)-Hapa wamemkataa Nyerer na Karume na wanawagombanisha wakati wamekufa.Ni nai asiyejua msimamo na mwelekeo wa Mwl. Nyerer?
Wapo wanasiasa wenye matamanio yao (Self personal Interest)ambao wanataka madaraka. Kiongozi anatangaza vita ila yeye na mkewe wamejifungia ndani. Hivyo wa kuumia ni Wananchi tu.
Marais watakao watawala watawatawala ninyi na watoto wenu, hebu tutazame maslahi ya taifa na si chama na tusishabikie mambo tusiyoyajua. Hebu tuunde Tume (Commision) sote tuwe na Katiba huru zitakazo tuongoza, sivyo wagawane muda wa maongozi yaani miaka miwili na nusu. Waongoze kwa zamu na uwe Muungano katika serikali mbili na si tatu.
Tuwe na mambo ya pamoja
1.Udugu sote tunahitajiana na soe tunandugu pande zote.
2. Jeshi ni lazima tuangalie yanayotokea Somalia, Nigeria na Kongo hivyo tunapaswa kuwa makini sana,
3. Sarafu moja
4. Ardhi
5. Bunge la Muungano
.
No comments
Post a Comment