Writen by
sadataley
4:43 PM
-
0
Comments
"Yesu anatuita tuwe Wamisionari ni sisi sote tulioitwa kwa nafasi zetu , waamini wote na wale wanaotenda mema kwa wengine".
Papa Francis akizungumza na waamini pembeni amezungukwa na viongozi waandamizi wa Vatican.
Hayo yamesemwa na Papa Ffrancis alipokuwa akizungumza na waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro huko Vatikan.Baba Mtakatifu amesema sote(tunaoamini)tunaitwa na tunaalikwa kuwa Wamisionari kwa wengine kwani Yesu alipokuwa akiwatuma wale sabini na wawili(72)si kwamba sisi alitutenga hapana nasi tumealikwa kwa utume huo.
Papa francis amesema kuwa kwa upendo na wema wa Bwana wetu Yesu Kristo alitualika nasi tulioamini baada ya Mitume kwamba nasi tunapaswa kuwafanya wengine wamuone Mungu kupitia sisi. Hivyo basi kwakufanywa kuwa wafuasi (discipleship) tunapaswa kuonyesha ukuu na wema wa Mungu kwa wengine.Tunaposema kuonesha ukuu na wema wsa Mungu si kwa kuaa nao au kupoteza muda la bali ni kuwatangazia ukuu wa Ufalme wa Mungu.
Akifafanua zaidi Baba Mtakatifu amesema wale Mitume kumi na wawili (12 Disciples) wanawakilisha Maaskofu na wale sabini na wawaili (72) wanawakilisha watumishi wengine katika Kanisa na waamini wote ikiwa ni pamoja na wale wanaotenda matendo yote ya huruma.
Na siku zote nguvu za Mungu zi pamoja nasi "Shetani hana nguvu mbele ya Mungu"
No comments
Post a Comment