Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, August 1, 2013

THAILAND KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA UCHUMI KATIKA BARA LA AFRIKA

Na Leon Bahati
Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, amesema lengo la nchi yake ni kuhakikisha kuwa Tanzania inajiimarisha kiuchumi na kuwa kitovu cha kukuza maendeleo ya uchumi wa Bara la Afrika.
Shinawatra aliyasema hayo juzi usiku alipokuwa akizungumza katika dhifa ya Taifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete.
Kiongozi huyo ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu nchini, alisema uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili, unawafanya waone umuhimu wa kuifanya anzania kitovu cha maendeleo ya uchumi barani Afrika
Alisema uhusiano wa n chi hizi mbili, umekuwa ukikolezwa na misingi ya Serikali ya Tanzania ya kudumisha utawala bora na kukuza demokrasia.
Aliahidi kuwa mbali na mikataba mbalimbali ambayo ambayo Thailand imeingia, ili kuongeza uwekezaji na ukuzaji wa uchumi nchini, pia inakusudia kujiingiza katika vita dhidi ya malaria.
“Tutaunganisha nguvu zetu pamoja ili kupambana na malaria,” alisema Shinawatra kwenye dhifa hiyo iliyofanyika Ikulu, jijini    Dar es Salaam, baada ya mazungumzo baina ya viongozi hao wawili.
Katika mazungumzo yao, Thailand ilikubali kuisaidia Tanzania kukuza kiuchumi wake kwa kuwekeza kwenye sekta za nishati, afya, utalii, kilimo na madini.
Kwa upande wake, Rais Kikwete alieleza mambo mengine waliyokubaliana kuwa ni pamoja na Thailand kutoa nafasi kumi kwa Watanzania kwenda kusoma shahada ya uzamili katika fani mbalimbali.
Rais Kikwete alisema wafanyabiashara wa hapa nchini wamekuwa wakifaidika na uhusiano mzuri kati ya nchi hizi mbili na kusisitiza kuwa ujio wake utaendelea kukoleza fursa hiyo kwa Watanzania.
“Wafanyabiashara wa Tanzania wamekuwa wakiufahamu mji wa Bangkok kuliko hata wanavyofahamu miji mingine ya Tanzania kutokana na kuwepo kule mara kwa mara kwa shughuli za kibiashara,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema lengo la Serikali ni kuona kuwa wafanyabiashara wengi wa Tanzania wanatumia fursa hiyo kujiimarisha zaidi kiuchumi ili kuongeza ufanisi wa shughuli zao kwa manufaa yao na jamii za Kitanzania.
Juzi nchi hizi zilitiliana saini mkataba wa makubaliano ya kubadilishana wafungwa wa makosa yote waliofungwa katika magereza ya kila nchi.Mkataba mingine ni ya ukuzaji na ulinzi wa shughuli za uwekezaji, ushirikiano katika nyanja ya madini na ushirikiano katika masuala ya kiufundi ambao kwa upande wa Tanzania, ulisainiwa na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.
Thailand kwa upande wake, mikataba hiyo ilitiwa saini na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Surapong Tovichakochakul.
Thailand na Tanzania, zimekuwa na uhusiano mzuri wa muda mrefu na zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali za maendeleo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment