Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 24, 2013

Serikali yamkaanga raia wa Uswiss

. Yamnyang’anya umiliki wa ardhi aliyojipatia kinyemela
. Aliitumia kuuza viwanja kwa wageni kinyume cha sheria
. Raia wa Zimbabwe alishauziwa na kujenya nyumba
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imemnyang’anya raia wa Uswiss umiliki wa ardhi mkoani Tanga.
Mswiss huyo, Dk. George Hess, alidaiwa kumiliki kinyemela ardhi ya ufukwe wa Amboni uliopo Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.

Serikali imechukua hatua hiyo kwa maelezo kwamba Dk. Hess alikiuka Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kujipatia umiliki wa ardhi hiyo.

Dk. Hess anayeishi nchini Kenya, anadaiwa kumiliki ufukwe huo na kuuza viwanja kwa wageni na wazawa kinyume cha sheria za nchi.

Hatua hiyo ya Serikali imekuja baada ya JAMHURI kuandika habari kuhusu Dk. Hess na umiliki wa ufukwe huo, miezi mitatu iliyopita.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya wizara hiyo kililiambia JAMHURI kuwa uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha watendaji wa wizara hiyo miezi miwili iliyopita, jijini Dar es Salaam.

“Tumekaa kikao na tumemwita Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kaskazini, Doroth Wanzala na akatakiwa kutoa maelezo ambapo alikana kuhusika na utoaji wa kibali au hati ya umiliki wa ufukwe huo.

“Kikao kilikuwa ni kizito tumefanya hivyo kwa kuangalia mustakabali wa taifa kwani sheria iko wazi tulimsimamisha asifanye lolote katika eneo hilo na sasa tumeamua kumnyang’anya,” kimesema chanzo hicho.

Inaelezwa kuwa katika kikao hicho Wanzala alidai kupelekewa maombi ya kutaka Dk. Hess amilikishwe ufukwe huo na Ofisi Ardhi ya Halmshauri ya Walaya ya Muheza lakini alikaata kuyaidhinisha.

Chanzo hicho kilisema baada ya kukataliwa, Dk. Hess alianza kuuza viwanja hivyo bila idhini kwa madai kuwa yeye ni mmiliki halali wa kiwanja hicho.

Hata hivyo, JMHURI ilipomtafuta Msemaji wa Wizara hiyo, Abraham Nyantori,  ili kuzungumzia suala hilo ameeeleza kwamba kwa sasa hawezi kuzungumza lolote kuhusu hilo kwani watendaji wote wa wizara hiyo wanahudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma.

“Ni kweli tulikaa kikao kuhusu hilo lakini siwezi kuzungumza kwa sasa ndugu yangu, kwani makamishna wote ambao wangetoa majibu sahihi wako Dodoma, hata nikipiga simu sasa kuwauliza kuhusu hilo watanishangaa, wao wanazungumzia bajeti mie naleta mambo mengine, tutafutane kesho au baada ya bajeti nitakupa jibu kamili,” amesema Nyantori.

Dk. Hess, kupitia tovuti yake ya ambonibeach.com, alijitangazia ‘Jamhuri’ katika eneo hilo, kuwa ndiye mmiliki pekee Tanzania mwenye ufukwe, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999.

Sheria ya Mipango Miji namba 7 ya mwaka 2008 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004, inakataza mtu yeyote kumiliki ufukwe wa bahari bali fukwe zinapaswa kumilikiwa na umma. Lengo la kutungwa kwa sheria hiyo ni kuhakikisha fukwe hazihatarishi amani, ulinzi na usalama wa raia.

Pia sheria hizi zinalenga kupunguza uharibifu wa mazingira na kuwapa wananchi fursa ya kutumia fukwe za bahari kwa burudani, michezo na mambo mengine yenye tija nchini.

Mbali ya hilo, Dk. Hess pia kupitia tovuti hiyo, ametangaza kumiliki ardhi na kuiuza kinyume cha Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu cha 20 (1), kinachokataza wageni kumilikishwa ardhi ikiwamo ya maeneo ya ufukweni.


“Kuepusha mkanganyiko, mtu asiye raia [wa Tanzania] hapaswi kupewa ardhi isipokuwa kama ni kwa malengo ya uwekezaji chini ya Sheria ya Uwekezaji ya Tanzania ya mwaka 1977,”.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment