Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, July 28, 2013

Papa Francis awaonya wanasiasa waache ufisadi

                                                                                     Papa Francis 
Rio de Janeiro, Brazil. Papa Francis amewataka vijana kote duniani kushiriki katika harakati za kuubadili ulimwengu ili uondokane na dhana ya kuifanya siasa kuwa sehemu ya ufisadi badala ya huduma kwa jamii.
Katika salamu zake kwa vijana wanaohudhuria Siku ya Dunia ya Vijana inayofanyika mjini hapa, Papa Francis alieleza kuwa dunia ya leo imepoteza mwelekeo na kubakia ya matajiri kuogelea katika utajiri wao, wakimwaga chakula huku mamilioni wakilia na kuteseka kwa njaa.
Alisema matokeo yake, vijana wamepoteza imani kwenye taasisi za kisiasa zilizotawaliwa na rushwa, ufisadi na maovu.
Baada ya kuongoza maandamamo ya kilometa tatu njia ya msalaba, safari ya mwisho ya Yesu Kristo kabla ya kuteswa na kuwa msababani, Papa Francis alielezea kukerwa kwake kuhusu kupotea kwa utu wa mtu na ubaguzi wa rangi. Aliwaeleza maelfu ya vijana katika ufukwe wa Copa Cabana kwamba dunia inawategemea wao katika kuleta mabadiliko.
Katika safari yake, Papa Francis pia aliwapa wakati mgumu wanausalama, polisi wa Brazil baada ya mara kadhaa kuamuru gari lake la wazi lisimame huku yeye akiwabusu watoto wadogo na kuwashika mikono wengine.
Pia, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki alishuka kutoka kwenye gari lake mara kadhaa na kutembea kwa miguu kwenye safari hiyo ya umbali wa maili 1.8 huku wanausalama wakihangaika kumlinda. Kuhusu tatizo la njaa na uhalifu, alieleza kuwa binafsi hakubali wala kubariki maovu ya kudhalilishwa kama ilivyowahi kutokea kwa watoto ndani ya kanisa hilo miaka iliyopita.
Alielezea masikitiko yake juu ya kitendo cha jamii kuyafumbia macho maovu dhidi ya wasio na sauti au uwezo. Akizungumzia vijana waliopoteza imani kwa kanisa kutokana na kashfa mbalimbali, alisema mafundisho ya Injili na Ukristo ndio tiba kwao.
“Maumivu ya Kristo ambayo yameonekana pia hapa (Brazil) yatufumbue macho,” alisema Papa Francis na kuwataka vijana kujiamini badala ya kulalamikia matatizo yanayoendelea katika jamii.
Akiwa katika makazi ya watu maskini Alhamisi, aliwataka watu wenye uwezo kumaliza mgawanyiko baina yao na maskini.
Papa alikula chakula na vijana wakiwamo wafungwa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment