Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 27, 2013

MAMBO YALIVYOKUWA NDANI YA CCC UPANGA USIKU WA KUAMKIA LEO

Usiku wa kuamkia leo ndani ya kanisa la kisasa nchini la City Christian Centre (CCC) Upanga jijini Dar es salaam kumefanyika tamasha la usiku wa kuabudu (Night of Worship) ambao ulikuwa wa aina yake na kubariki wengi waliohudhuria ambapo Mungu alijichukulia utukufu baada ya watu zaidi ya 10 kumpa Yesu maisha yao pamoja na kufanyika maombi ya kuwafungua watu kutoka katika vifungo mbalimbali yaliyoongozwa na askofu mkuu wa pili mstaafu wa T.A.G Renwall Mwanisongole ambaye ndiye mchungaji kiongozi wa kanisa hilo.

Vikundi vilivyoongoza watu katika kumsifu Mungu ni pamoja na The Next level, Neema Gospel Choir (N.G.C) kutoka AIC Chang'ombe ambao uimbaji wao umebadilika sana kutokea upigaji hadi uimbaji kwa ujumla na kubariki wengi waliohudhuria kanisani hapo, pia kulikuwa na vikundi vingine vingi ambavyo vilifanyika baraka kwa mamia ya waliofika katika usiku huo wa kuabudu.








Habari picha na Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment