Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, July 18, 2013

LENGO KUU LA ZIARA YA PAPA FRANCIS HUKO BRAZIL IKIHUSISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI.

Safari ya Papa Francis ya kwenda Brazil  ni kwaajili ya siku ya Vijana Duniani ijulikanayo kama World Youth Day (WYD) mwezi huu julai tarehe 25.
Pope Francis will arrive in Brazil on July 25 (AP)
             pope francis apanga ziara ya kwenda Brazil mnamo mwezi julai mwaka huu.
Ziara hiyo iliyopangwa na Papa Francis ambayo atatembelea huko Brazil ni kwa ajili ya siku ya vijana Duniani ijulikanayo kama WYD (WORLD YOUTH DAY) Tarehe 25 mwezi huu wa julai
WYD itafanyika katika mji wa Rio de Janeiro kutoka Julai 22-28, pia Baba Federiko Lombardi alizungumza waziwazi wakati akiwa katika mkutano uliofanya na waandishi wa habari juu ya maelezo ya kuaandaa  ratiba kwaajili ya ziara ya Papa Francis.
Mipango kwa ajili ya safari ya Papa ya kwenda katika mji huo wa Rio de Janeiro ilikuwa imeshaanza kupangwa  chini ya Papa Benedict XVI. Tarehe ya safari Papa Francis 'ni sawa, na siku ambayo Baba Mtakatifu atawasili Brazil mnamo Julai 25, ingawa baadhi ya mabadiliko yamefanywa na ratiba ya Papa  Francis ikiwa ni pamoja na  kuondoa siku moja bila ya mapumziko na kuongeza matukio kadhaa kama vile: kufanya ziara kwa Parokia ya Mama yetu wa Aparecida, ziara ya hospitali  kwa watumishi masikini na wale waloweza kupata nafuu kutokana na kuathiriwa na madawa ya kulevya, na pia kufanya mkutanona na kamati ya uratibu wa baraza la Maaskofu wa Amerika Kusini '.
Papa pia atatembelea Manguinhos katika makazi wanayoishi watu wenye hali duni zaidi ikiwemo ni ya kiafya, ambapo atakuwa akishughurikia jamii kutoka maeneo hayo pembezoni mwa barabara katika viwanja vya mpira  vya mjini hapo. Baba Lombardi aliongeza kwamba Papa Francis pengine ataweza kuongeza Hotuba kwenye mkutano huo ambao tayari imeshawekwa juu ya Julai 27 akiwa pamoja na  makardinali wa Brazil na Maaskofu kutoka Rio na mikoa jirani.

Hakuna hata jambo moja ambalo Papa Francis atashindwa kulifanya, hata hivyo, ataitisha mkutano wakati atapokuwa njiani kuelekea mjini humo kwa masaa 12, japokuwa hakupanga kuwasiliana na wawakilishi 71 watakao wakilisha waandishi wa vyombo vya habari juu ya bodi hiyo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment