Writen by
sadataley
7:48 PM
-
0
Comments
MRADI HUO UNATARAJIA KUANZA MAPEMA MWEZI UJAO NA UTAWANUFAISHA ZAIDI YA WATU 170 KWA AWAMU YA KWANZA.MRADI HUO UNATARAJIWA KUTEKELEZWA KATIKA SHARIKA ZA KILOLO NA KILENGA PASI (LUGANGA).
MCHUNGAJI YONA KINGANGA
MCHUNGAJI KIONGOZI USHARIKA WA KILOLO
Hayo yamesemwa na Mchungaji Yona Kinganga pichani akisema kuwa mradi huo wa mbuzi unatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao. Akiendelea kutoa maelezo amesema kuwa jumla ya mbuzi 175 zitagawiwa huku majike yakiwa ni mia moja sabini (170) na madume matano (5). Walengwa watakao nufaika na mradi huo ni wajane, yatima na wagane toka katika sharika mbili Usharika wa Kilolo na Usharika Mpya wa Kilengapasi(Luganga) ambao kwa kweli Kanisa limeridhia na kuona wanahitaji kupewa nafasi ya kuingizwa katika mradi huo.
Mchungaji Kinganga alitoa mkazo kuwa ni watu mia moja sabini watakaoanza na ni wale wasio na uwezo kabisa huku wakiwa na wajibu wa kusomesha watoto.
Mradi huu ni sehemu ya matunda ya mahusiano ya Usharika wa Kilolo na Swideni na kwamba siku ya Jumamosi hii( 20/07/2013) itafanyika semina elekezi katika usharika huo ambapo wawezeshaji ni shirika la Navigator toka Morogoro.
Na pia akasema kuwa maandalizi ya mabanda ya kufugia yamekwisha anza na tayari walishapewa ramani inayoelekeza namna ya kujenga.
Mfano wa banda la kufugia mbuzi likiwa katika hatua za mwisho kukamilika
No comments
Post a Comment