Writen by
sadataley
9:33 AM
-
0
Comments
Matukio ya ugaidi Polisi waomba ushirikiano wa viongozi wa dini
Na Joseph Lyimo, Mwananchi
Mirerani. Kufuatia vitendo vya kigaidi vinavyoendelea nchini, Mkuu wa Kituo cha Polisi Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Ally Mohamed Mkalipa ametoa wito kwa viongozi wa madhehebu ya dini wa mji mdogo huo kuanzisha vikundi vya amani na ulinzi katika maeneo yao.
Akizungumza juzi na viongozi wa madhehebu ya dini wa mji mdogo wa Mirerani, Mkalipa alisema lengo la kuanzisha vikundi hivyo vya watu watano ni kuhakikisha uwapo wa amani kupitia ulinzi na usalama katika maeneo ya ibada.
Alisema baada ya viongozi wa madhehebu kwenye makanisa na misikiti kuchagua watu watano watakaounda kikundi cha ulinzi na usalama kwenye maeneo yao, amani na usalama itakuwapo kwenye wa nyumba hizo za ibada.
“Wanaweza kuweka ulinzi usio na bughudha kwa waumini, lakini watakuwa wanachukuwa tahadhari endapo kuna mtu amebeba kitu ambacho siyo cha kawaida, katika sehemu za ibada ili kibainike ni kitu gani,” alisema Mkalipa.
Alidai kuwa endapo kikundi cha watu watano kitakuwa kinafanya ulinzi kwenye maeneo ya madhehebu, amani na usalama itakuwepo na endapo kutakuwa na tukio lolote hatarishi,watatoa taarifa kituo cha polisi au kwa maofisa watendaji.
Pia, aliwataka viongozi hao wa madhehebu kutoa taarifa ya ujio wa ugeni nyeti katika eneo hilo.
No comments
Post a Comment