Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, June 17, 2013

Bajeti haina unafuu kwa walalahoi, wasema wananchi

Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akiingia bungeni Dodoma jana kusoma hotuba ya Bajeti. Picha na Fidelis Felix. 
Na Burhani Yakub,, Mwananchi 
Tanga. Bajeti ya Serikali ilyosomwa Alhamisi iliyopita na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa imezidi kukosolewa kwamba inalenga katika kuwanyonya wananchi wa kipato kidogo na kuwanufaisha vigogo.
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na Utawala Bora  ya jijini Tanga, Ashery Vurugu, alisema ni bajeti isiyokuwa  na huruma kwa walalahoi.
Alisema Serikali imeweka msamaha wa kodi ya pikipiki za bodaboda, lakini wakati huohuo imepandisha bei ya petroli, jambo ambalo alisema ni kuwaumiza wananchi.
“Leseni ya barabara  ni mara moja tu kwa mwaka, lakini mafuta ni kila siku sasa Serikali inapopandisha bei ya mafuta na kusema imewawekea mazingira mazuri watu wa pikipiki inamaanisha nini,”alisema Vurugu.
Alisema bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/14  ni ya kuwanyamazisha midomo wabunge ili wasizungumzie kasoro zake, lakini ifahamike kwamba ni wawakilishi wa wananchi ambao kupandishiwa bei ya mafuta ni kuwakamua hata kile kidogo walichonancho.
Aliwataka wabunge watakapoanza kuichambua bungeni, kuhakikisha kuwa mianya ya ukwepaji kodi kwa wafanyabiashara wakubwa na  wawekezaji, inazibwa.
Bajeti hiyo iliyosomwa sambamba na bajeti za serikali zingine  za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, imelalamikiwa na wananchi wakidai kuwa hailengi katika kuwapa unafuu wa maisha. Wanalalamikia bei ya petroli.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment