Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, June 17, 2013

WATU 5000 KUHUDHURIA JUBILII YA MIAKA 50 YA
KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA
21-24 JUNI, 2013
CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA 

Bw.Brighton Kilewa
Katibu Mkuu K.K.K.T
Katibu Mkuu wa KKKT Bw. Brighton Kilewa amesema watu 5000 wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya jubilii. Wageni wapatao 5,000 wanatarajiwa kuhudhuria matukio ya kilele cha jubilii ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) tarehe 22 na 23 Juni 2013 kukumbuka miaka 50 tangu Makanisa saba ya Kilutheri nchini kuungana na kuunda Kanisa moja. Katibu Mkuu wa KKKT, Bw. Brighton Killewa alisema hivi karibuni,  kilele kitaadhimishwa katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (Tumaini University Makumira -TUMA), Usa River kinachomilikiwa na KKKT kitakuwa na matukio ya siku mbili.

Alisema Juni 22 litakuwepo kongamano ambapo mada tano zitajadiliwa kuhusu kazi za Kanisa miaka 50 iliyopita na nini kifanyike kwa miaka 50 ijayo.
 Siku ya Jumapili 23 Juni ndipo itafanyika Ibada. Tarehe 21 jioni Mkuu wa KKKT anatarajiwa kufungua maonyesho ya kazi mbalimbali na usiku kutakuwa na mkesha wa kwaya yenye watu 350.

Kanisa linatarajia wageni wapatao 5,000 toka ndani na nje ya nchi kuhudhuria maadhimisho hayo yatakayofanyika Usa River, nje kidogo ya jiji
 la Arusha. Wageni wa nje ni kutoka makanisa na vyama vya misioni vya  Afrika, Ulaya na Marekani. Kutoka ndani ni pamoja na wawakilishi waDayosisi za KKKT, viongozi wa Serikali na wa dini na kwaya.

Chuo cha Makumira ni mojawapo ya vituo vya pamoja kama Kanisa (vijulikanavyo kama vituo vya Kazi za Umoja KKKT) kinachounganisha Dayosisi zote 22 za KKKT. Ni kituo cha mafunzo kilichoanza kama chuo cha Theologia hivyo viongozi wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki, Kati, Kusini na Magharibi mwa Afika na Mashariki ya Mbali (Middle East) wakiwemo Wachungaji na Maaskofu wamesoma katika chuo hicho. Chini ya mpango wa kubadilishana wanafunzi baadhi ya wanafunzi na wakufunzi wametoka Ulaya na Marekani.

KKKT ni muungano wa makanisa saba ambayo baadhi yao yalianza kutekeleza utume wa Mungu wa kueneza Injili nchini zaidi ya miaka 150. Tarehe 19 Juni
 1963 viongozi wa Makanisa hayo saba kwa hiari yao waliweka tofauti zao

kando na kuamua kuunda Kanisa moja na kugeuza Makanisa yao kuwa Sinodi au Dayosisi za KKKT.Kadiri muda ulivyokwenda KKKT ikakubaliana kuacha mfumo wa Sinodi na kuwa na mfumo wa Dayosisi.

Hadi 26 Mei 2013 Dayosisi za KKKT zimefikia 22 baada ya mbili kuzinduliwa mwaka huu wa Jubilii. Nazo ni Dayosisi ya Kusini Mashariki (Mtwara/ Lindi) iliyozinduliwa Jumapili 26 Mei 2013 na Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga/ Simiyu) iliyozinduliwa 5 Mei2013.
Habari  na Elizabeth Lobulu-Afisa Habari K.K.K.T
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment