Writen by
sadataley
2:00 PM
-
0
Comments
MATUKIO NA HABARI PICHA KATIKA KUSIMIKWA KWA ASKOFU WA
DAYOSISI YA KUSINI MASHARIKI 26.05.2013
Muonekano wa Madhabahu ya Kanisa Kuu la K.K.K.T-Dayosisi ya Kusini Mashariki
Katibu Mkuu wa K.K.K.T Bw. Brighton Kilewa akisoma hati tayari kuruhusu Askofu Mteule kusimikwa kuwa Askofu huku kiti cha Askofu kikiwa bado kimefunikwa
Askofu Mteule akiwa amesimama mbele tayari kwa kusimikwa kuwa Askofu
Akivishwa Msalaba kama alama ya Upendo aliouonesha Bwana Wetu Yesu kristo alipojitoa pale Msalabani kwa ajili yetu
Askofu Mbedule akivalishwa Pete ili imkumbushe kuwa mwaminifu kwa Mungu wake na pia imkumbushe kuuhifadhi umoja na kuheshimu patano lake na Kanisa lake Mungu.
Askofu Mbedule akivalishwa Joho kama kumbukumbu na alama ya upana wa kazi uliyoitwa na Bwana katika Kanisa lake
Askofu akipewa kofia kama alama ya Ukuhani wake Yesu Kristo katika Kanisa lake
Askofu Mbedule akiokea fimbo kama alama ya Mchungaji Mwema anayefia kondoo zake.
Askofu mbedule akiwa tayari Askofu kamili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
Askofu Mbedule akitumwa rasmi kwenda kufanya kazi kama Askofu wa K.K.K.T
Katibu Mkuu akisoma hati ya Kumruhusu Mkuu wa Kanisa kumuingiza kazini
Askofu Mbedule kuwa Mkuu wa Dayosisi ya Kusini Mashariki
Mkuu wa kanisa Dkt. Alex Malasusa akimtangaza rasmi Askofu Mbedule kuwa Mkuu wa Dayosisi ya Kusini Mashariki
Kiti cha Askofu kikiwa tayari kwa kutumiwa na Askofu wa Kwanza wa
Dayosisi ya Kusini Mashariki
Askofu Mbedule akiwa tayari katika kiti cha Uaskofu
Askofu Mbedule akimuingiza kazini msaidizi wake
Waimbaji wa Kwaya Kuu K.KK.T-Dayosisi ya Iringa wakifuatilia ibada hiyo
Hongera na karibu kwa kazi ya Bwana ni maneno ya Msaidizi wa Askofu Mchg. Mwakihaba toka Dayosisi ya Konde (Mbeya)
Baadhi ya wachungaji toka Dayosisi mbalimbali wa kutoka kulia ni Mchg.Moses Matimbwi na nyuma yake ni Mchungaji Adela Kivelege ambaye kwa sasa ni Mchumgaji wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani huku Mchungaji Gudaga toka dayosisi ya Kusini mwenye kitabu akisikiliza kwa umakini
Waziri Mkuu akisikiliza kwa umakini salam za Kanisa kwa Serikali
Askofu Ngonyani wa Jimbo la Lindi akitoa salam toka Kanisa Katoriki
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Newala, Oscar Mnung’a akitoa salam toka Kanisa hilo
"Serikali ipo tayari kushirikiana nanyi nasi tunawategemea kuhubiri Amani na Upendo na kuwataka waheshimu viapo vyao" ni maneno ya Waziri Mkuu kwa Maaskofu wote wa K.K.K.T
Ahsanteni sana kwa kushirikiana nasi ni maneno ya Mkuu wa Kanisa Dkt.Alex Malasusa kwa Waziri Mkuu hayupo pichani
Twende kazini sasa ni maneno yanayoonekana kusemwa kimoyoni na Msaidizi wa Askofu Mbedule
Mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wakiwa na Maskofu wa K.K.K.T huku Askofu Mbedule akiwa na fimbo yake na pembeni ni mwenzi wa Askofu Mbedule
Mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mkuu wa Kanisa , Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakiwa na Askofu Mbedule, Msaidizi wake, wenzi wao na baadhi ya wasidizi wa Maaskofu toka Dayosisi MbalimbaliMgeni rasmi Waziri Mkuu, Mkuu wa Kanisa wakiwa na Askofu Mbedule, Msaidizi wake na wenzi wao
Baadhi ya wawakilishi toka vyama rafiki na K.K.K.T wakiwa na baadhi ya Wakuu wa Majimbo na kwa waliosimama ni mama Mchg. Kiwanga toka iringa akifuatiwa na Mkuu wa Jimbo Mchg.Donald Kiwanga
MGENI RASMI AKIWA NA BAADHI YA MAKATIBU WAKUU WA DAYOSISI ZA K.K.KT
waliosimama wa kwanza kutoka kushoto ni Bw. Nayman Chavalla-Iringa Dayosisi na Barozi Maliki wa Mashariki na Pwani
IFUATAYO NI BAADHI YA MAMBO YALIYOSEMWA NA WAZIRI MKUU KATIKA HOTUBA NA SALAM ZA SERIKALI KATIKA TUKIO HILO
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema wawekezaji 45 wameomba kuwekeza Mtwara baada ya kugundulika kwa gesi asilia mkoani humo.
Akizungumza katika sherehe za kusimikwa kwa Askofu wa Kanisa la KKKT, Dayosisi ya Kusini Mashariki, Lucas Mbedule jana Mjini Mtwara, Pinda alisema uwekezaji huo utaiwezesha Mtwara kupaa kiuchumi ndani ya miaka 10 ijayo.
“Hadi sasa kituo cha uwekezaji kina maombi takriban 45 ya wawekezaji mkoani Mtwara, ikiwamo kiwanda cha mbolea, bidhaa za plastiki… vyote hivi vitakuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi kwa wananchi wa Mtwara na Taifa kwa jumla, hususan katika ajira,” alisema Pinda.
Alisema Serikali inafahamu kuwa upo umuhimu mkubwa wa kuleta maendeleo ya nchi kwa uwiano bila kubagua kwa misingi ya jinsia, rangi, kabila, dini, mikoa au ukanda… “Maendeleo ya nchi kwa uwiano ni nguzo muhimu kwa umoja na mshikamano wa wananchi wa taifa husika kama Tanzania.”
Alisema zipo nyakati ambazo baadhi ya wananchi mmojammoja au kwa makundi kama vile, jinsia, rangi, kabila, dini, mikoa na kanda wamekuwa wakiamini kuwa wanaachwa nyuma kimaendeleo na kwamba hali hiyo inasababishwa na kusubiri kwa muda mrefu na kutokupata taarifa sahihi kuhusu malengo na mipango iliyopo ya kuleta maendeleo.
No comments
Post a Comment