Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, March 19, 2018

UN yaunga mkono kufanyika uchaguzi Julai nchini Zimbabwe

Umoja wa Mataifa umesema kuwa unaunga mkono mpango wa kufanyika uchaguzi wa rais nchini Zimbabwe mwezi Julai mwaka huu.
Achim Steiner, Mkuu wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNDP ambaye alikuwa katika safari rasmi ya kikazi mjini Harare hapo jana na kukutana na Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo, amesema umoja huo unaunga mkono kikamilifu mchakato wa maandalizi ya uchaguzi wa mwezi Julai, sambamba na jitihada serikali za kuinua uchumi wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
Baada ya kukutana na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini mjini Harare jana usiku, Rais Mnangagwa alisema Wazimbabwe watakuwa na fursa ya kumchagua kiongozi wao mwezi Julai mwaka huu, na wala sio mwezi Agosti kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali.
Phillipe Van Damme, Mkuu wa Umoja wa Ulaya nchini Zimbabwe amesema anapanga kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Mnangagwa, viongozi wa vyama vya siasa na wakuu wa Tume ya Uchaguzi kesho Jumatatu kuhusu uchaguzi huo ujao.
Emmerson Mnangagwa, aliyekuwa makamu wa Rais wa Zimbabwe alifutwa kazi na Robert Mugabe na kwenda uhamishoni Afrika Kusini kabla ya kurejea nchini humo na kuchaguliwa na Bunge kuwa rais wa nchi hiyo.
Parstoday.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment