Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, March 17, 2018

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 17.03.2018

Lewandowsk huenda akajiunga na Real madrid katika dirisha kubwa la usajili

Image captionLewandowsk huenda akajiunga na Real madrid katika dirisha kubwa la usajili
Real Madrid imekubali kusajili mshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland Robert Lewandowski.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 29 pia anafuatiliwa na klabu za Chelsea na Manchester United.(Mundo Deportivo )
Mlinzi wa kati wa Real Madrid Raphael Varane amesema Manchester United inamuhitaji. Mfaransa huyo mwenye miaka 24 alisajiliwa klabuni hapo chini ya Jose Mourinho.(Cadena Ser, via Sun)
Kiungo wa zamani wa Liverpool na Bayern Munich Dietmar Hamann amesema Bayer wanazungumza na kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino juu ya uwezekano wa kuwanoa.(Sky, via Mirror)
Jack Wilshare yuko katika mawindo ya Everton
Image captionJack Wilshare yuko katika mawindo ya Everton
Everton iko tayari kumlipa kiungo wa Arsenal Jack Wilshere ambaye mkataba wake na Gunners unaisha mwisho wa msimu huu.Wapo tiyari kumpa paundi milioni 8 kwa mwaka iwapo atasajiliwa bure.(Times )
Borussia Dortmund wameonyesha nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Westham mreno Domingos Quina.(Sun)
Spurs wanatarajia kufanya mazungumzo ya kumpa mkataba mpya mshambuliaji raia wa Korea Kusini Son Heung-min.Mkataba wake wa sasa unaishia mwaka 2020.(Sky Sports)
Michael Appleton yupo miongoni mwa makocha wanaowaniwa na West Brom
Image captionMichael Appleton kuwanaowaniwa na West Brom
Meneja msaidizi wa Leicester city Michael Appleton yupo miongoni mwa makocha wanaowaniwa na West Brom kuziba nafasi ya Alan Pardew.(Telegraph)
Mlinda mlango wa Roma Alisson anahusishwa kujiunga na Liverpool lakini matamanio yake ni kwenda Real Madrid.(Express)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema mlinzi wa kati Gary Cahill na mshambuliaji Alvaro Morata wanahitaji juhudi zaidi iwapo wanataka kurejea katika kikosi cha kwanza na kuweka uwezekano wa kuziwakilisha timu zao za taifa ambazo ni Uingereza na Hispania.(Express)
Conte anaamini hawezi ondolewa kwenye klabu ya Chelsea iwapo mabingwa hao wa msimu uliopita hawatafuzu kucheza klabu bingwa ulaya msimu ujao.(Telegraph)
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment