Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, March 5, 2018

Simba yaomba msaada Azam FC


Klabu ya soka ya Azam FC imeweka wazi kuwa haina mahusiano yoyote na timu a Al Masry, ambayo imetua nchini leo kwaajli ya kucheza na Simba huku ikitumia Basi la klabu hiyo kutoka Uwanja wa ndege kuelekea hotelini.

Akiongea na wanahabari msemaji wa Azam FC Jaffary Idd Maganga amesema kuwa kutoa Basi ni sehemu ya biashara ya klabu hivyo kwa timu yoyote ambayo inahitaji huduma hiyo ifuate tu taratibu zote na itapata Bus.

''Basi ni sehemu ya biashara ya timu na sio mara ya kwanza kutumika hata timu ya taifa huwa inatumia mara nyingi tu kama ilivyo kwa uwanja wetu, na uongozi wa Simba umeandika barua kwa CEO na wamepewa lakini hatuna mahusiano na Al Masry'', amesema.

Al Masry imetua leo nchini tayari kwa mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao Simba siku ya Jumatano Machi 7 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment