Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, March 5, 2018

Korea Kaskazini yaionya Marekani

Korea Kaskazini imetoa onyo kwa Marekani kuwa haitobembeleza kufanya mazungumzo na nchi hiyo.

Korea Kaskazini imesema ipo tayari kuingia vita na Marekani na haitakubali mazungumzo yoyote na Marekani yaliyowekewa masharti.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Pyongyang ni kwamba Korea Kaskazini ilikuwa na nia ya kufanya amzungumzo ya kidiplomasia na Marekani lakini haipo tayari kutimiza masharti ya aina yoyote ile.

Korea Kaskazini imeisisitizia Marekani kuwa isijidanganye wala kufikiria mambo mengine baada ya nchi hiyo kutaka kufanya mazungumzo na Marekani.

Marekani na Korea Kaskazini zimekua katika mvutano baada ya Korea Kaskazini kuanza kufanya majaribio ya makombora ya nyuklia. Korea Kaskazini imeonekana kuwa ni tisho kubwa kwa Marekani.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment