Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, March 17, 2018

Rais Trump na Moon waijadili Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump amezungumza na rais wa Korea Kusini Moon Jae In kuhusu mkutano wake na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Viongozi hao wawili katika mazungumzo hayo wamesisitiza kuwa endapo Korea Kaskazini itachagua njia iliyo sahihi basi kutakuwa na mustakabali mzuri kwa taifa hilo.

Kwa mujibu wa habari,Trump na Moon wanaamini kuwa vitendo na sio maneno ndio vinavyohitajika kusuluhisha masuala ya Korea Kaskazini na majaribio yake ya makombora ya nyuklia.

Endapo mkutano huo utafanyika utakuwa ni wa kwanza kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini na rais wa sasa wa Marekani.

Mkutano unatarajia kufanyika mwisho wa mwezi Mei.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment