Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, March 5, 2018

Mwanamume ajipiga risasi na kujiua nje ya White House

Police outside the White House front lawn - 3 March 2018


Image captionPolisi nje ya White House
Mwanamume mmoja amejipiga risasi na kujiua nje ya Ikulu ya Marekani ya White House mjini Washington, kikosi cha kumlinda rais kimesema.
Kikosi hicho kilisema kuwa mwanamume huyo alikaribia ua unaozunguka Ikulu katika barabara ya Pennsylvania kabla ya kuchomoa bunduki na kupiga risasi mara kadhaa.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa, kulingana na polisi. Rais Donald Trump hakuwa kwenye Ikulu. Yuko katika kasri lake la Mar-a-Lago huko Florida.
People running at the White HouseHaki miliki ya pichaTWITTER/@FLORIANLUHN/VIA REUTERS
Image captionVideo iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter ilionyesha watu wengi wakikimbia kutoka eneo hilo
Mwanamume huyo alikuwa kwenye watu wengi wakati alipiga risasi, kulingana na wale walioshuhudia.
Video iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter ilionyesha watu wengi wakikimbia kutoka eneo hilo.
Jina na mtu huyo bado halijatangazwa. Kumekuwa na visa kadha vinavyohusu usalama katika Ikulu ya White House miaka ya hivi karibuni.
Cha hivi karibuni tarehe 23 Februari, gari liliendeshwa kwenda kwa kizuizi cha Ikulu ambapo mwanamke wa miaka 35 alikamatwa.
Tourists mill outside the north fence of the White HouseHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKisa hicho kilitokea karibu ua wa Ikulu

BBC

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment