Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, March 5, 2018

IS wasambaza picha za video za mauaji

Video zilizosmbazwa na IS


Image captionVideo zilizosmbazwa na IS
Wapiganaji wa kundi la Islamic State IS wamesambaza picha za video zinazodaiwa kuonyesha mauaji ya wanajeshi wane wa Marekani waliouawa nchini Niger mwezi Octoba mwaka mwaka jana.
Hata hivyo haijajulikana mara moja kwanini picha hizo zimetolewa kwa kuchelewa hadi, ambapo zimetolewa kupitia program ya kimtandao ya Telegram
Picha hizo zilipigwa na mmoja wa wanajeshi wa Marekani kupitia kamera yake ya siri aliyokuwa nayo kwenye kofia yake ngumu aliyokuwa ameivaa yaani Helmet.
Lengo la video hizo ni kutaka kubainisha kwamba IS ndiyo waliofanya shambulio hilo.
Picha zinazo onekana zinaanza na zile za mnato ambazo baadhi ya wapiganaji hao wakitoa kiapo cha utii kwa kiongozi wao Abu Bakr al-Baghdadi mtandao huo wenye makundi yenye utiifu kwa IS kama vile Sahel, Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM).
Kwa mjibu wa BBC video hizo zinawaonyesha wapiganaji hao wakitembea na kukimbia jangwani kuelekea kufanya shambulizi.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment