Matokeo ya awali yanayoendelea kutangazwa nchini Sierra Leone, yanaonesha kuwa mgombea wa upinzani anaongoza dhdi ya mgombea wa chama tawala kwa zaidi ya kura elfu 15.
Mgombea wa upinzani Julius Maada Bio amepata asilimia 43.5 ya kura dhidi ya asilimia 42.6 alizopata mgombea wa chama tawala Samura Kamara huku tume ya uchaguzi ikiwa imehesabu karibu asilimia 75 ya kura zote.
Muungano wa kitaifa unaoongozwa na mwanadiplomasia wa zamani kwenye umoja wa Mataifa Kandeh Yumkella ambaye anatarajia kugawa kura za wagombea vinara hao yeye amepata asilimia 6.69 ya kura zote.
Matokeo rasmi ya uchaguzi uliofanyika juma lililopita yanatarajiwa kutangazwa ndani ya siku chache zijazo lakini kwa matokeo haya ni wazi kuwa huenda kukawa na duru ya pili ya uchaguzi kwa kuwa hakuna mgombea ambaye huenda akafikisha ushindi wa asilimia 55 inaotakiwa kikatiba.
No comments
Post a Comment