Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, March 2, 2018

Hali ya hewa yazidi kuwa tatizo barani Ulaya

Hali mbaya ya hewa imeendelea kuleta taharuki katika eneo kubwa la Bara la Ulaya, ambapo watu kadhaa wamekufa na mamia ya nyumba kukosa umeme kufuatia hali mbaya ya baridi iliyofikia nyuzi joto ya chini ya sifuri.

Nchini Ireland usafiri wa aina mbalimbali pamoja na ule wa ndege umeahirishwa kufuatia upepo mkali uliosababishwa na dhoruba kali iliyoziacha nyumba takribani 24,000 na maeneo ya biashara kukosa umeme wakati nchini Uingereza maelfu wakikumbwa na giza.

Barafu inayomiminika katika nchi hizo imesababisha hali ya maisha kuwa ngumu kwa wasafari na wananchi kwa jumla.

Tahadhari imeendelea kutolewa kwa wananchi huku kwa wasio na makazi, wakipatiwa hifadhi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment