Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, March 2, 2018

Al Shabab wawateketeza Polisi watano nchini Kenya

Polisi watano wameuawa nchini Kenya baada ya kushambuliwa na magaidi wa Al Shabab kutoka Somalia, wakiwa katika kambi yao katika Kaunti ya Mandera Kaskazini mwa nchi hiyo.
Shambulizi hilo lilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa kwa mujibu wa afisa wa serikali katika Kaunti hiyo Eric Oronyi ambaye amesema, magaidi hao walivamia kambi mbili za Polisi hao katika mji wa Fino.
Aidha, Oronyi amesema magaidi hao walikuwa kati ya 70 na 100 na waliwasili katika kambi hiyo wakitembea kwa mguu, iInaelezwa kuwa, polisi waliokuwa wanalinda malango ya kambi hizo mbili, walilemewa na kuwawezesha magaidi hao kuingia katika kambi hizo.
Mbali na mauaji hao, Polisi wengine watatu wamejeruhiwa na kusafirishwa kwenda kupata matibabu jijini Nairobi., Magaidi hao pia wameharibu mtambo wa simu ya Safaricom kabla ya shambulizi hilo.
Kenya imeendelea kukabiliwa na tishio la Al Shabab tangu mwaka 2011, ilipotuma wanajeshi wake nchini Somalia.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment